SHALOM IMEKUKWISHA TAYAARIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!



Ubatizo mwingine Nbii patimo akifanya ubatizo katiza ziwa victoria mwanza huu ndio wakati wa kumgeukia Bwana Mungu wako






 


WARAKA WA KINABII JUU YA MADHABAHU YA BWANA KATIKA NCHI YA TANZANIA


MKAWAFANYE MATAIFA YOTE KUWA WANAFUNZI WANGU MKIWABATIZA KWA JINA LA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU























WARAKA WA KINABII JUU YA MADHABAHU YA BWANA KATIKA NCHI YA  TANZANIA ,NABII PATIMO

Wakati huu Bwana ameongea tena juu ya kanisa lake lililotekwa na uovu na machukizo ya kila namna na ya kwambaBwana anaona wivu sana juu ya madhabahu yake inayozidi kuchafuliwa siku hadi siku ,na sasa yeye aliye mwanzo na mwisho Mungu mkuu muumbawa  mbingu na nchi Mungu wa Isaka ,Ibrahim na Yakobo  Yehovah Sabaothi,Yehovah Nisi ,Yehovah Ellgibo,Yehovah Markadeshi .
Amenituma kwako kwa waraka huu wa kinabii Ee kanisa la Tanzania hata lini utageuka na kumrudia Bwana Mungu wako?
Usiku wa leo tarehe 8/12/2013 Bwana akanichukua katika Roho mtakatifu macho yangu yakafunguka nami nikaona makundi mawili ndani ya nchi moja yaani sekali halali na serikali ya watu walioasi ,ndipo nikaona wakitafuta namna ya kupatana ikashindikana kabisa.vita ikatokea ndipo Bwana akanichukua tena mpaka mahali pasiri,nami nikaona tukio hilo lililo sababisha taharuki ndani ya Nchi ya Tanzania nami niokaona watanzania wakiingia katika makambi ya wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe kutokea upande wa kaskazini ,kusini na mashariki,katika hayo maono macho yangu ya roho yakafunguka zaidi nikaona wingi wa miiba ikiwachoma walio kuwa wakikimbia vurugu hizo na tazama ndani ya hiyo miiba nikaona wadudu wenye rangi ya brauni wenye vichwa vigumu na vikali misili ya misumari  ikiwangata wale walionusurika na ile miiba na katika  hayo maumivu makali sana Bwana akanionyesha madhabahu yake,nikaona maji yaliyokuwa kwenye ndoo yako nusu juu ya madhabahu .
Ndipo nikasikia sauti ikiniambia oga,oga,oga,nami nilipo oga nikasikia sauti ya mwanamke(kanisa)ikishangaa yakwamba nimewezaje kuonga !Ndipo Bwana akaniambia liambie kanisa langu lioge na kujitakasa maana kanisa langu limetekwa na uovu na machukizo ya kila namna ,tena Bwana  akanichukuatena katika Roho nami nikaona wakati na majira ya kurudi kwake mwana wa Mungu na harusi ya mwana kondoo ikiwa tayari maandalizi yake Bwana akanionyesha kwa mfano wa saa ya kibinadamu ili nipate kuelewa zaidi nikaona mshale wa dakika ukiwa arobaini na tano maana yake kasoro robo.
Natena nikaona vazi jeupe sana likiwa tayari kwajili ya tukio la harusi ya mwanakondo nikawaona malaika wa Bwana wakiwa tayari kwajili hiyo,lakini Bwana harusi alipotazama bibi harusi wake (kanisa)akakuta ametekwa na ndio maana ya ilesauti ya mwanamke (kanisa)iliyokuwa ikinishangaa nikioga ,ndipo nikauona wivu mkuu wa Bwana juu ya bibi harusi wake (kanisa )aliyetekwa Bwana akasema nami kama alivyo nane kwa kinywa cha Nabii Sefania 6:8,Basi ningojeeni asema Bwana hata siku ile nitakapo ondoka kuteka mateka .maana nimeazimia kuwakusanya mataifa ili nizikusanye falme nipatekuwamwagia gadhabu yangu naam,ukali wote wa  hasira yangu kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu
Bwana anakuja kukomboa kanisa lake lililotekwa na uovu amegiza toba ya kweli na yakumaanisha juu ya madhabahu yake maana anakuja upesi ,wewe uliyepata waraka huu wa kinabii chukua hatua ya kutubu sasa ,la sivyo wakati Bwana atakapoiadhibu nchi ole wao makuhani wasimamao katika madhabahu iliyotekwa na uovu kwa maana Bwana atakapoichukua mateka ya madhabahu yake iliyotekwa na uovu hao makuhani wataangamizwa pamoja na uovu huo uliokidhiri katika madhabahu kwakuwa wivu mkuu wa Bwana umewaka juu ya madhabahu yake .
Heri hao watubuo na kuoshwa dhambi zao kwa damu ya mwana kondoo tena heri roho itubuyo asema Bwana wa majeshi.
Nabii Patimo www.trbimtz.org +255762946327 ,The rivers of breakthrough international ministries

walikuwa hawatembei sasa wanatyembea uamusho mkuu umetokea tanzania






UAMUSHO MKUU KUTOKE TANZANIA ULIO GAWANYIKA MARA 3


Tarehe 31/1/205 saa tisa alfajiri nilipokuwa katika Roho mtakatifu macho yangu ya roho yalifunguka nami nikaliona kanisa la Bwana katika nchi ya Tanzania likiwa katika hali ya ukiwa na kujikunyata kanisa amabalo limesinyaa kanisa amabalo halina mamlaka kabisa,nikiwa katika hali ya kuendelea kulitazama kanisa Bwana akaniambi lete mkono wako nami nilipofungua kiganja changu cha mkono akaniwekea vitu viwili vidogo vyenye mfano wa vidonge vya priton kisha akaniambia kunja kiganja chako  halafu tembea


Nilipoanza kutembea vile vitu viliwaka moto ndani ya mkono wangu naye akasema kaza mwendo nilipo kaza mwendo navyo vikazidi kuwaka zaidi akaniambia kwa sauti kuu kimbiiaaa nilipokimbia vikalipuka mlipuko mkuu katika mkono wangu naye akaniambie mwaga huo moto katika ardhi ya Tanzania nami nikafanya hivyoo,akaniambia huu ni uamusho mkuu unakwenda kutokea kwa mkono wangu mwenyewe ni uamusho ambao hapana mtu yeyote awezaye kuubeba kwa mkono wake isipokuwa ni kwa mkono wangu mwenyewe .


Baada ya hapo niliendelea kutembea katika njiaa hiyohiyo ya kanisa ndipo nikaona uamusho wa pili ambao ni uamusho wa uponyaji wa magonjwa sugu ,Bwana akanionyesha kwa mfano wa kapu kubwa sana lililo jaa aina flani ya matunda ukitaza kwamfano wa kibidamu yanafanana na machungwa lakini ni makubwa sana akaniambia chukua ule nilipochukua hayakuwa na ladha yoyote mwanzoni hivyo sikumaliza nikatupa inje ya lile kapu akaniambia chukua jingine ule nami nilipochukua nikaanza kula kwambali nilihishi ladha flani mdomoni mwangu baada ya hapo akanimbia huu ni uamusho wa uponyaji wa magojwa sungu na tena amelikumbuka kanisa na watu masikini ambao hawana pesa za kufuata tiba katika inchi za mbali yohana 6:30 .


 Nilipo endelea mbele kidogo nikama nilishuka katika bode flani nami nikakuta mvua kubwa sana  nabaada ya hiyo mvua nikaona majengo makubwa sana ya kuabudi na tena nikaliona kusanyiko kuu likiabudu Mungu katika Roho na kweli na katika uweza mkuu wa Mungu .


Nabii patimo www.trbimtz.org




























women deliverd from the powers of Darkness

Mhe: Nabii akiwafungua watu katika mkutano mkubwa wa kinabii Kateshi manyara

SIKU 90 ZA TOBA KWAJILI YA TANZANIA





Shalom Tanzania ,napenda kusema kwamba huu ni wakati wa kwenda mbele za Mungu kama taifa kwa toba juu ya nchi yetu ya tanzania Mungu amekuwa akisema nami marakwamara juu ya toba kwa taifa sawasa na kitabu cha ezekiel 14:1-14 katika hayo maandiko tunajifunza pamoja na kuona jinsi ambavyo Mungu anasema juu ya Taifa ambalo limetenda dhambi ya kuabudu Sanamu pamoja na Vinyago vya kila namna kwahiyo yako mambo mengi sana ambayo yumefanya kama Taifa vitu hivyi vimesimama mbele za Mungu kama vinyago na ibada ya sanamu kwa leo sitavitaja lakini wewe chukua hatua hii ya kutubu kwajili ya nchi.2nyakati 7:12-14