KUSUDI LA ZIARA YA NABII NA MTUME DK PATIMO KATIKA NCHI YA TANZANIA NA AFRICA KWA UJUMLA


Kusudi la Ziarala  ya Nabii dk patimo katika nchi nzima ya Tanzania pamaja na mataifa 52 ya Africa,25 /4/2012. nilikuwa katika Roho ndipo nikaona na tazama ninapika chakula kingi sana na wakati nikiendelea ghafla niliona kusanyiko kubwa sana lililo kuwa likisubisi chakula hicho,nakatika kutazama kusanyiko hilo niliona makundi mawili ndani yakusanyiko hilo.kundi la kwanza lilikuwa na watu walio konda sana na wadhaifu sana nao hawakuwa wengi sana kundi la pili ambalo ndilo lililokuwa kubwa watu wake walikuwa wamekufa ,katika kuendelea kutama hayo makundi huku pia nikiendelea kupika kile chakula na baada ya chakula kile kuiva ndipo nikalia sana katika Roho kwani walio paswa kula hawakuwa wanajiweza kwani wengine wamekufa,na wengine wana hali ngumu sana.katika hali hiyo nikiwa katika Roho nikalia juu ya wale walio kufa ghafla walianza kuinuka na kujikongoja mahali nilipokuwa ni kiomba na kila aliyenigusa bega langu  alitiwa nguvu tena wote waliamka kwa kutiwa nguvu mpya ya ajabu.
katika hali hiyo nami nikamuuliza Bwana nini maana ya maono haya? ndipo neno la Bwana likanijia  mwanangu hili ni kanisa langu liko katika hali ya kufa na udhaifu mwingi ,nami ninakutuma wewe kuachilia ufufuo na nguvu ya uamsho juu ya kanisa langu africa ikiwepo Tanzania 'kwahiyo baada ya ujumbe huo wa kinabii nilianza ziara hizo ambazo tunaandaa makongamano ya maombi ya nchi nzima ya Tanzania hadi sasa tumesha maliza mikoa 5 pamoja na wilaya zake na tunaendelea hadi tumalize kusudi la kinabii ambalo Mungu ametupa,ujumbe huu umewekwa hapa kwa lengo la kuweka bayana madhumuni ya ziara ya Nabii Daniel katika africa nzima na pia kwa wale ambao ni wana maombi waendelee kuomba juu ya nchi yetu pamoja na Africa kwa ujumla wake.Mungu ibariki Africa ,Mungu Ibariki Tanzania kumbuka ni ruhusa kutoa maoni yako na tutayafanyia kazi,umebarikiwa katika Jina la Bwana Yesu.