PROPHECY

UNABII JUU YA AJALI MWEZI WA SITA






Tarehe 9/6/2016  Bwana alimpa Nabii wake neno la kinabii kwa habari ya Ajali itakayolikumba Taifa la Tanzania na Nbii aliwataka watu kuomba juu ya Taifa ili kuepusha Roho ya ajali lakini watu walipinga na kumpiga mawe ya Maneno siku saba tu baada ya unabii




UNABII JU
AJALI YA MOTO.MNAMO 17/9/2014 MAJIRA YA 16.00 HRS HUKO KIJIJI CHA NG'ALILE (W) RUANGWA (M) LINDI KATIKA BARABARA YA NANGANGA - RUANGWA, GARI LA ABIRIA NO.T417BNH YOUTONG MALI YA BALAJ TRANSPORT IKIENDESHWA NA ATHUMANI RASHID CHONGWE MWENYE UMRI WA MIAKA50 KABILA MZARAMO  MKAZI WA BUGURUNI D'SLAAM LILIUNGUA MOTO NA KUTEKETEA KABISA.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAKIJAJULIKANA. HAKUNA MADHARA KWA ABIRIA WALA MALI ZAO.
ajali ya pili siku tisa baada ya unabii


Basi la NBS linalotoka DAR kwenda TABORA limepata ajali mbaya maeneo ya Gairo Morogoro. Watu 4 wafariki na 10 kujeruhiwa katika ajali

ya basi la NBS.

Huku ajali nyingine ya basi la KISBO likijeruhi watu kadhaa Morogoro. Basi la Kisbo T895CYL Limepata ajali ya kuparuzana na trailer flatbed eneo la Magubike Kilosa.
siku 21 baadaye 

U YA ARUSHA. OLE WAKO EE KANISA LA ARUSHA UNANI WEWE HATA KUDHIRA NA KUONDOKA MBELE ZA BWANA?????

Tarehe 27/2/2015 saa 11 asubuhi nikiwa Mwanza wilaya ya Magu bwana alinichukua katika Roho mpaka Arusha ndipo akanionyesha jinsi ambavyo

Watu 30 wafariki kwa ajali ya gari Singida

Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili ya City Boy eneo la Maweni mkoani Singida





Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili ya City Boy eneo la Maweni mkoani Singida.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka amesema ajali hiyo imehusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea Dar es Salaam kwenda Kahama na basi namba T 247 lililokuwa likitokea Kahama kwenda Dar es Salaam.
Aidha metaja mabasi hayo ni mali ya kampuni ya City Boys ambapo yamegongana uso kwa uso na kuua abiria 24 papo hapo na wengine sita kufariki baadaye na wengine kujeruhiwa na kueleza kuwa idadi ya majeruhi na vifo vitaendelea kutolewa.
kanisa la arusha lilikuwa mbele zake lakini lilikuwa limedhira yaani limemkataa bwana wakati nikiwa katika hayo maono na tazama nikaliona kanisa la Bwana nimeondoka mbele za Bwana yaani limeacha njia yake.Ndipo nikaiona gathabu ya Bwana imewaka juu ya Arusha nikamwona Bwana akiunyoosha mkono wake wa hasira kali juu ya Arusha tena nikasikia Sauti ikiuliza wako wapi wachungaji wa Arusha? Nami sikuwaona ila niliona watu waliokuwa hawazidi wato wakiwa wamelala chini kifudifudi wakiomboleza juu ya Arusha.

Siku ya tarehe 8/3/2015 yaani siku tisa baada ya tarehe 27 nikiwa katika ibada ya kinabii magu mwanza nikasema tena Bwana anakwenda kuipiga arusha kwa gathabu yake maana tayari mkono wa Bwana ujuu ya arusha ,tena nimeona moto mkuu umeachiliwa juu ya arusha ,siku moja baadaye yaani siku ya tarehe 9 saa tisa mchana Bwana akathibitisha maneno ya kinywa changu kwa kupiti ITV breaking news ,nukuu ya ITV zaidi ya migodi 15 mererani  arusha imeteketea  kwa moto na zaidi ya watu 1500 hawana kazi na wengine zaidi ya 1000 hawana makaazi,unabii huu ambao Bwana Jehovah amenionyesha umetimia ni kweli kwamba hatafanya jambo lolote bila kuwajulisha watumishi wake Manabii

Hatahivyo tunawapole watu wa arusha pamoja na serikali ya mkoa huo lakini nitakuja arusha maana Bwana anataka kanisa la Arusha lirudi mbele zake. Shalom Nabii patimo.




Unabii juu ya kufariki kwa Mhe.capten Jonh Komba


Tarehe 14.2.2015 Nabii wa Mungu patimo akiwa katika dhiara ya kinabii katika mkoa wa kagera wilaya ya karagwe kata ya kayanga majira ya saa tisa alfajiri Bwana alimuonesha maono ya msiba huo na haya ndiyo yalikuwa maneno yake aliyowaambia waombaji waliokuwa wakiomba Dodoma kwajili ya nchi na taifa kwa ujumla kupitia kwenye simu ya askofu mama Kimonge 0763452034 

shalom mtumishi tafadhali ombeni juu ya hili nimeona msiba wa kitaifa yaani kiongozi amefariki tena nimeona bendera ya taifa juu ya jeneza .tarehe 27 mwezi wa pili yaani siku 14 baada ya unabii wa Nabii wa Mungu patimo unabii ukatimia taifa likaomboleza kifo cha kiongozi maarufu wa kisiasa na kitaifa ambaye sana alijulikana kwa kipawa chake cha uimbaji, nikweli kabisa hakuna jambo litakalo tokea katika taifa au mataifa pasipo Bwana kumjulisha nabii wake .hatahivyo huduma ya mito ya upenyo inayoongozwa na Nabii wa Mungu patimo inapenda kutoa pole sana kwa familia ya hayati mhe, capten john komba ni kweli kabisa kwamba taifa pia limempoteza mtu muhimu sana .Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la BWANA libarikiwe Amen






UAMUSHO MKUU KUTOKE TANZANIA ULIO GAWANYIKA MARA 3

Tarehe 31/1/205 saa tisa alfajiri nilipokuwa katika Roho mtakatifu macho yangu ya roho yalifunguka nami nikaliona kanisa la Bwana katika nchi ya Tanzania likiwa katika hali ya ukiwa na kujikunyata kanisa amabalo limesinyaa kanisa amabalo halina mamlaka kabisa,nikiwa katika hali ya kuendelea kulitazama kanisa Bwana akaniambi lete mkono wako nami nilipofungua kiganja changu cha mkono akaniwekea vitu viwili vidogo vyenye mfano wa vidonge vya priton kisha akaniambia kunja kiganja chako  halafu tembea

Nilipoanza kutembea vile vitu viliwaka moto ndani ya mkono wangu naye akasema kaza mwendo nilipo kaza mwendo navyo vikazidi kuwaka zaidi akaniambia kwa sauti kuu kimbiiaaa nilipokimbia vikalipuka mlipuko mkuu katika mkono wangu naye akaniambie mwaga huo moto katika ardhi ya Tanzania nami nikafanya hivyoo,akaniambia huu ni uamusho mkuu unakwenda kutokea kwa mkono wangu mwenyewe ni uamusho ambao hapana mtu yeyote awezaye kuubeba kwa mkono wake isipokuwa ni kwa mkono wangu mwenyewe .

Baada ya hapo niliendelea kutembea katika njiaa hiyohiyo ya kanisa ndipo nikaona uamusho wa pili ambao ni uamusho wa uponyaji wa magonjwa sugu ,Bwana akanionyesha kwa mfano wa kapu kubwa sana lililo jaa aina flani ya matunda ukitaza kwamfano wa kibidamu yanafanana na machungwa lakini ni makubwa sana akaniambia chukua ule nilipochukua hayakuwa na ladha yoyote mwanzoni hivyo sikumaliza nikatupa inje ya lile kapu akaniambia chukua jingine ule nami nilipochukua nikaanza kula kwambali nilihishi ladha flani mdomoni mwangu baada ya hapo akanimbia huu ni uamusho wa uponyaji wa magojwa sungu na tena amelikumbuka kanisa na watu masikini ambao hawana pesa za kufuata tiba katika inchi za mbali yohana 6:30 .

 Nilipo endelea mbele kidogo nikama nilishuka katika bode flani nami nikakuta mvua kubwa sana  nabaada ya hiyo mvua nikaona majengo makubwa sana ya kuabudi na tena nikaliona kusanyiko kuu likiabudu Mungu katika Roho na kweli na katika uweza mkuu wa Mungu .

Nabii patimo www.trbimtz.org


WARAKA WA KINABII JUU YA MADHABAHU YA BWANA KATIKA NCHI YA  TANZANIA ,NABII PATIMO












Wakati huu Bwana ameongea tena juu ya kanisa lake lililotekwa na uovu na machukizo ya kila namna na ya kwambaBwana anaona wivu sana juu ya madhabahu yake inayozidi kuchafuliwa siku hadi siku ,na sasa yeye aliye mwanzo na mwisho Mungu mkuu muumbawa  mbingu na nchi Mungu wa Isaka ,Ibrahim na Yakobo  Yehovah Sabaothi,Yehovah Nisi ,Yehovah Ellgibo,Yehovah Markadeshi .
Amenituma kwako kwa waraka huu wa kinabii Ee kanisa la Tanzania hata lini utageuka na kumrudia Bwana Mungu wako?
Usiku wa leo tarehe 8/12/2013 Bwana akanichukua katika Roho mtakatifu macho yangu yakafunguka nami nikaona makundi mawili ndani ya nchi moja yaani sekali halali na serikali ya watu walioasi ,ndipo nikaona wakitafuta namna ya kupatana ikashindikana kabisa.vita ikatokea ndipo Bwana akanichukua tena mpaka mahali pasiri,nami nikaona tukio hilo lililo sababisha taharuki ndani ya Nchi ya Tanzania nami niokaona watanzania wakiingia katika makambi ya wakimbizi ndani ya nchi yao wenyewe kutokea upande wa kaskazini ,kusini na mashariki,katika hayo maono macho yangu ya roho yakafunguka zaidi nikaona wingi wa miiba ikiwachoma walio kuwa wakikimbia vurugu hizo na tazama ndani ya hiyo miiba nikaona wadudu wenye rangi ya brauni wenye vichwa vigumu na vikali misili ya misumari  ikiwangata wale walionusurika na ile miiba na katika  hayo maumivu makali sana Bwana akanionyesha madhabahu yake,nikaona maji yaliyokuwa kwenye ndoo yako nusu juu ya madhabahu .
Ndipo nikasikia sauti ikiniambia oga,oga,oga,nami nilipo oga nikasikia sauti ya mwanamke(kanisa)ikishangaa yakwamba nimewezaje kuonga !Ndipo Bwana akaniambia liambie kanisa langu lioge na kujitakasa maana kanisa langu limetekwa na uovu na machukizo ya kila namna ,tena Bwana  akanichukuatena katika Roho nami nikaona wakati na majira ya kurudi kwake mwana wa Mungu na harusi ya mwana kondoo ikiwa tayari maandalizi yake Bwana akanionyesha kwa mfano wa saa ya kibinadamu ili nipate kuelewa zaidi nikaona mshale wa dakika ukiwa arobaini na tano maana yake kasoro robo.
Natena nikaona vazi jeupe sana likiwa tayari kwajili ya tukio la harusi ya mwanakondo nikawaona malaika wa Bwana wakiwa tayari kwajili hiyo,lakini Bwana harusi alipotazama bibi harusi wake (kanisa)akakuta ametekwa na ndio maana ya ilesauti ya mwanamke (kanisa)iliyokuwa ikinishangaa nikioga ,ndipo nikauona wivu mkuu wa Bwana juu ya bibi harusi wake (kanisa )aliyetekwa Bwana akasema nami kama alivyo nane kwa kinywa cha Nabii Sefania 6:8,Basi ningojeeni asema Bwana hata siku ile nitakapo ondoka kuteka mateka .maana nimeazimia kuwakusanya mataifa ili nizikusanye falme nipatekuwamwagia gadhabu yangu naam,ukali wote wa  hasira yangu kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu
Bwana anakuja kukomboa kanisa lake lililotekwa na uovu amegiza toba ya kweli na yakumaanisha juu ya madhabahu yake maana anakuja upesi ,wewe uliyepata waraka huu wa kinabii chukua hatua ya kutubu sasa ,la sivyo wakati Bwana atakapoiadhibu nchi ole wao makuhani wasimamao katika madhabahu iliyotekwa na uovu kwa maana Bwana atakapoichukua mateka ya madhabahu yake iliyotekwa na uovu hao makuhani wataangamizwa pamoja na uovu huo uliokidhiri katika madhabahu kwakuwa wivu mkuu wa Bwana umewaka juu ya madhabahu yake .
Heri hao watubuo na kuoshwa dhambi zao kwa damu ya mwana kondoo tena heri roho itubuyo asema Bwana wa majeshi.Nabii Patimo www.trbimtz.org +255762946327 ,The rivers of breakthrough international ministries